Ikiwa wewe au rafiki yako yuko katika ndoa ya kulazimishwa au una wasiwasi utalazimika kuolewa, tafadhali jua kuwa msaada unapatikana na kwamba wewe hauko peke yako.
Huenda ukaogopa na usijue kuhusu maisha yako ya baadaye, na umechanganyikiwa kuhusu hisia zako na majukumu yako. Unaweza kupata msaada kwa kupigia namba mojawapo kwenye ukurasa huu.
Haijalishi umri wako ulivyo; nchi gani au historia ya familia unayotokea; iwe ni mume au mwanamke; au utamaduni wako au dini yako – hakuna mtu anayeruhusiwa kukushinika kuolewa kinyume na mapenzi yako.