Mwanzo

Ikiwa uko katika ndoa kwenye ndoa ya kulazimishwa au una wasiwasi utalazimishwa kuolewa, tafadhali jue kwamba msaada unapatikana na kwamba hauko peke yako.

Huenda ukaogopa na usijue maisha yako ya baadaye, na kuchanganyikiwa kuhusu hisia zako na majukumu yako. Unaweza kupata msaada kwa kuwasiliana na nambari mojawapo ya simu kwenye ukurasa huu.

Haijalishi umri wako ulivyo; nchi gani au historia ya familia unayotokea; iwe ni mume au mwanamke; au utamaduni wako au dini yako – hakuna mtu anayeruhusiwa kukushinika kuolewa kinyume na mapenzi yako.

Ikiwa unahitaji ushauri, unaweza kupiga simu (02) 9514 8115 au tuma barua pepe kwa help@mybluesky.org.au au tuma ujumbe kwa 0481 070 844. Tunaweza kukusaidia kupata mtasfsiri ikiwa unamuhitaji.

Je unajisikia siyo salama? Ikiwa kuna dharura au unaumizwa unaweza kupiga zero tatu (000) kutoka kwa simu yoyote.

Nini maana ya ndoa ya kulazimishwa?

Ndoa ya kulazimishwa ni wakati mtu anapata ndoa bila kukubaliana kwa hiari na kikamilifu. Hii inaweza kuwa kwa sababu hawaelewi asili na athari za sherehe ya ndoa au wamefungwa, kutishiwa au kudanganywa. Hii inaweza kuhusisha shinikizo la kihisia kutoka kwa familia zao, vitisho, au madhara halisi ya kimwili, au kufanyiwa udanganyifu katika kuolewa na mtu fulani. Aina hii ya ndoa ina athari mbaya kwa muda mrefu kwa watu na familia na ni kinyume cha sheria nchini Australia.

Pakua kupata maelezo zaidi kuhusu ndoa ya kulazimishwa hapa chini.

Banner
Locker Room

The Locker Room

Close