Nini maana ya ndoa ya kulazimishwa?

Nini maana ya ndoa ya kulazimishwa?

Ikiwa uko katika ndoa ya kulazimishwa au una wasiwasi kuwa utalazimishwa kuolewa, tafadhali jua kuwa msaada unapatikana na kwamba wewe hauko peke yako. Unaweza kuwa na hofu na kutokuwa na uhakika wa maisha yako ya badaye. Unaweza kuchanganyikiwa juu ya hisia na majukumu yako na huenda usijue kitu cha kufanya baadaye. Unaweza kupigia mojawapo ya nambari kwenye ukurasa huu ili kupata msaada na usaidizi.

Ndoa ya kulazimishwa ni wakati mtu anapoolewa bila kukubaliana kwa hiari na kikamilifu. Hii inaweza kuwa kwa sababu hawaelewi asili na athari za sherehe ya ndoa au wameweza kutishiwa au kudanganywa, kwa sababu ya shinikizo la kihisia kutoka kwa familia zao, vitisho au madhara halisi ya kimwili, au kufanyiwa udanganyifu wa kuolewa na mtu mwingine. Ikiwa mtu ana umri wa chini ya miaka 16 wakati wa kuolewa, kwa kawaida hachukuliwi kuwa anaweza kukubaki kwa uhuru na kikamilifu kuolewa. Aina hii ya ndoa inaweza kuwa na athari mbaya kwa muda mrefu kwa watu na familia na ni kinyume cha sheria nchini Australia.


KWA HABARI ZAIDI KUHUSU SHERIA NCHINI AUSTRALIA BONYEZA HAPA

Mnamo Machi 2013 sheria ilianza kutekelezwa ya kufanya ndoa ya kulazimishwa kuwa kinyume cha sheria nchini Australia. Ni uhalifu kumfanya mtu aingie katika ndoa ya kulazimishwa au kuweza kuhusika katika ndoa ya kulazimishwa (isipokuwa kama wewe ndie unayeteswa). Sheria imejumuishwa katika Idara ya 270 ya Sheria ya Makosa ya Jinai ya Kisheria Kutaifa ya 1995. Makosa yanachukua kiwango cha juu cha jela ya miaka 7, au miaka 9 kwa kosa la kuchochea, ambalo ni pamoja na kulazimisha mtu aliye chini ya umri wa miaka 18 kuolewa au kulazimisha mtu mwenye ulemavu kufunga ndoa. Kama mtu akisaidia kupanga kwa mtoto wa chini ya umri wa miaka 18 kuchukuliwa nje ya Australia na kuolewa, anaweza kuwekwa jela kwa muda mpaka miaka 25.


Kama uko kwenye ndoa ya kulazimishwa

… au una wasiwasi kama kulazimishwa kuolewa, tafadhali jua kuwa msaada unapatikana na kwamba hauko peke yako. Unaweza kuwa na hofu na bila kuwa na uhakika maisha yako ya baadaye. Unaweza kuchanganyikiwa juu ya hisia na majukumu yako na huenda usijue cha kufanya baadaye. Unaweza kupigia namba mojawapo kwenye ukurasa huu ili kupata msaada na usaidizi.

Mifano ya ndoa za kulazimishwa

1.’Msichana mwenye umri wa miaka 17 ana mpenzi lakini wazazi wake wanamwambia kuwa lazima asimamishe kumwona ili aolewa na mtu mwingine. Anaambiwa kwamba ikiwa hakubali kuolewa na mtu mwingine, atakuwa na madhara. Kama msichana huyo akiendelea mbele na ndoa hiyo kwa sababu anaogopa kuumizwa, hii ni ndoa ya kulazimishwa. ‘

Mifano ya ndoa za kulazimishwa

2.’Msichana mwenye umri wa miaka 15 anaambiwa kwamba anaenda likizo ya familia wakati wa likizo za shule. Wakati yeye na familia yake wanapofika nje ya nchi anaambiwa kwamba lazima aolewe na binamu. Anaambiwa kwamba ikiwa hatakubaliana na kufanya ndoa hawezi kuruhusiwa kurudi Australia. Ikiwa ndoa hiyo ikiendelea mbele hii inakuwa ndoa ya kulazimishwa. ‘

Mifano ya ndoa za kulazimishwa

3. ‘Mwanaume mwenye miaka 19 anaambia familia yake kuwa ni shoga. Wiki chache baadaye, familia yake inamwambia kwamba lazima amwoe mwanamke mdogo katika jamii aliyoijua kwa miaka mingi. Ndoa inakwenda mbele kwa sababu anaambiwa kwamba ikiwa hawezi kumuoa, ataleta aibu nyingi katika familia yake na kwamba bibi yake anaweza kupatwa na ugojwa wa  moyo. Hii ni ndoa ya kulazimishwa. ‘

NINI MAANA YA NDOA YA KUPANGILIA?

Katika familia zingine, ndoa zinapangwa. Wanandoa huletwa kwa wajumbe wa familia au mtu mwingine. Kila mtu anaweza kuchagua kwa uhuru ikiwa wanataka kuendelea na ndoa na familia zao husikiliza uchaguzi wao bila matokeo yoyote  mabaya. Ndoa za kupangwa zinakubalika kisheria nchini Australia kwa watu zaidi ya umri wa miaka 18 kwa sababu wanandoa wanaolewa tu ikiwa wote wawili wakiamua kuoana.

Hata kama wao wakikubaliana kwanza, ndoa ya kupangwa inaweza kubadilika kuwa ndoa ya kulazimishwa ikiwa mtu mmoja au wote wawili wanatishiwa, wamelazimishwa au kushinikizwa kusema ndiyo ili kuoana. Mtu anaweza kujisikia kutokuwa na uwezo wa kusema hapana kwenye harusi. Wakati huo, hawatatoa ridhaa kamili na huru hivyo ndoa inakuwa ya kulazimishwa.

BONYEZA HAPA KUONA MFANO WA NDOA ZA KUPANGILIA

Mtu mwenye umri wa miaka 19 anatambulishwa kwa ndugu wa familia ambaye ambaye anaweza kuoana naye, rafiki au mtu mwingine. Mtu huyo anaweza kuchagua kusema ‘ndiyo’ au ‘hapana’ kwenye ndoa. Ikiwa wanaamua kusema ‘hapana’ kuweza kuoana, haitaweza kuendelea. Ikiwa wanaamua kusema ‘ndiyo’ kuweza kuoana kwa idhini yao kamili na bila kulazimishwa, ndoa itaendelea. Idhini yao kamili na bila kulazimishwa inamaanisha kwamba hakukuwa na vitisho, mitego au shinikizo juu yao ili kusema ndiyo kwenye kuoana.

Banner

USALAMA WA KOMPTUTA NA SIMU

Hakikisha kuwa uko katika mahali salama kwa kutumia simu salama au kompyuta ili usiweze kufuatiwa au kufuatiliwa. Ikiwa una wasiwasi kuhusu usalama wako, unaweza kukopa simu ya rafiki yaklo au kutumia kompyuta kwenye maktaba ya umma au kituo cha jamii.

Ikiwa unahitaji kuondoka kwenye tovuti hii haraka, bofya kitufe cha ‘kutoka kwenye tovuti’ kwenye kona ya juu ya mkono wa kurasa. Hii itakwenda moja kwa moja kwenye ukurasa wa utafutaji wa Google ulio wazi lakini haitafungua historia ya kivinjari chako.

Locker Room

The Locker Room

Close